1
Mungu atukuzwe, kwa mambo makuu, Upendo wake ulitupa Yesu, Aliyejitoa maisha yake, Tuwe nao uzima wa milele.
Kiitikio
Msifu, msifu, dunia sikia, Msifu, msifu watu wafurahi, Na uje kwa Baba, kwa Yesu Mwana, Ukamtukuze kwa mambo yote.
2
Wokovu kamili, zawadi kwetu, Ahadi ya Mungu kwa ulimwengu, Wanaomwamini na kuungama, Mara moja wale husamehewa.
3
Alitufundisha mambo makuu, Alihakikisha wokovu wetu, Lakini zaidi ajabu kubwa, Yesu atakuja na tutamwona.