21

Baba Twakujia

1

Baba twakujia, uwe msaada, Uwe kimbilio, twakusihi, Dunia ni giza, tukitengwa nawe, Tufariji hapa, Baba yetu.

Kiitikio

Baba twakujia, tu dhaifu, na usituache, tusikie.

2

Salama tulinde, kati ya taabu, Uwe raha yetu, mashakani. Roho yasumbuka, Baba tujalie, Twakuomba sana, tupe nguvu.

3

Neema utupe, tukubali kwako, Moyo wetu linda, safarini, Tuongoe mbele, tupate kushinda, Na kufika ng’ambo, kule kwako.