1
Usinipite Mwokozi, unisikie, Unapozuru wengine, usinipite.
Kiitikio
Bwana, Bwana, unisikie, Unapozuru wengine, usinipite.
2
Kiti chako cha rehema, nakitazama, Magoti napiga pale, nisamehewe.
3
Sina ya kutegemea, ila wewe tu, Uso wako uwe kwangu, nakuabudu.
4
Wewe tu u Mfariji, sina mbinguni, Wala duniani pote, Bwana mwingine.