1
Yesu furaha ya moyo, hazina ya pendo na nuru. Yote yatupendezayo, yasilinganishwe nawe.
2
Kweli yako ya daima, wawajibu wakwitao, Ni siku zote u mwema, kwao wakutafutao.
3
U Mkate wa Uzima, kupokea ni baraka, Twanywa kwako u kisima, roho zikiburudika,
4
Mwokozi twakutamani, kwako roho hutulia, Twakushika kwa imani, nawe watubarikia.
5
Yesu, ndiwe kwetu mwanga, tufurahishe daima, Giza la dhambi fukuza, uwe mwanga wa Uzima.