1
Jina lake Yesu tamu, tukilisikia, Hutupoza tena hamu, hutuondolea.
2
Roho iliyoumia, kwalo hutibika, Chakula njaani pia, raha tukichoka.
3
Jina hili ni msingi, ngao, ngome, mwamba, Kwa hili napata vingi, kwangu ni akiba.
4
Yesu, Mchunga, Rafiki, Mwalimu, Kuhani, Mwanzo, Mwisho, na Amina, mali yangu yote!
5
Moyo wangu hauwezi, kukusifu kweli, Ila sifa zangu hizi, Bwana zikubali.