1
Taji mvikeni, taji nyingi sana, Kondoo mwake kitini, Bwana wa mabwana, Nami tamsifu, kanifia mimi, Ni Mfalme mtukufu, Bwana wa mbinguni.
2
Taji mvikeni, Mwana wa Bikira; Anazovaa kichwani, aliteka nyara, Shilo wa manabii, Mchunga wa watu, Shina na tanzu ya Yese, wa Bethlehemu.
3
Taji mvikeni, Bwana wa Mapenzi; Jeraha zake ni shani, ni vito vya enzi, Mbingu haina, hata malaika, Awazaye kuziona, pasipo kushangaa.
4
Taji mvikeni, Bwana wa salama, Kote-kote duniani, vita vitakoma, Nayo enzi yake, itaendelea, Chini ya miguu yake, maua humea.