1
Tutokapo tubariki, utupe kufurahi, Tuwe na pendo lako, neema ya kushinda. Nawe utuburudishe, tukisafiri chini.
2
Twatoa sifa shukrani, kwa neno la Injili, Matunda yake wokovu, yaonekane kwetu, Daima tuwe amani, kwa Kweli yako Bwana.
3
Siku zeku zikizidi, tuzitoe kwa Yesu, Tuwe na nguvu moyoni, tusichoke njiani, Hata tutakapoona, Utukufu wa Bwana.