1
Tena Mwokozi twalitukuza, Jina lako lenye kupendeza, Twangojea neno la amani, Kabla hatujakwenda nyumbani.
2
Tupe amani njiani mwetu, Wewe u mwanzo u mwisho wetu, Dhambini kamwe isiingie, Midomo ikutajayo wewe.
3
Utupe amani usiku huu, Ili gizani kuwe nuru kuu, Tulinde kwa kuwa kwako Bwana, Usiku ni sawa na mchana.
4
Tupe amani ulimwenguni, Ndiyo dawa yetu majonzini, Na ikitwita sauti yako, Tupe amani milele kwako.