28

Jina Lake Yesu Tamu

1

Jina lake Yesu tamu, lihifadhi moyoni, Litakufariji ndugu, enda nalo po pote.

Kiitikio

Jina la thamani, (Jina la ) (thamani) Tumai la dunia, Jina la thamani, (Jina la thamani–tamu) Furaha ya mbinguni.

2

Jina la Yesu lafaa, kama ngao vitani, Majarabu yakisonga, omba kwa jina hili.

3

Jina hili la thamani, linatufurahisha, Anapotukaribisha, na tunapomwimbia.

4

Mwisho wa safari yetu, tutakapomsujudu, Jina hili tutasifu, furaha ya mbinguni.