29

Yesu Nakupenda

1

Yesu nakupenda u mali yangu, Anasa za dhambi sitaki kwangu, Na Mwokozi aliyeniokoa, Sasa nakupenda kuzidi pia.

2

Moyo umejaa mapenzi tele, Kwa vile ulivyonipenda mbele, Uhai wako ukanitolea Sasa nakupenda kuzidi pia.

3

Ulipoangikwa msalabani, Tusamehewe tulio dhambini, Taji ya miiba uliyoivaa, Sasa nakupenda kuzidi pia.

4

Mawanda mazuri na masikani, Niyatazamapo huko mbinguni, ‘Tasema na taji nitakayovaa, Sasa nakupenda kuzidi pia.