30

Yesu Unipendaye

1

Yesu unipendaye, kwako nakimbilia, Ni wewe utoshaye, mwovu akinijia. Yafiche ubavuni, mwako maisha yangu, Nifishe bandarini, wokoe moyo wangu.

2

Ngome nyingine sina, nategemea kwako, Usinitupe Bwana, nipe neema yako, Ninakuamania, mwenye kuniwezesha, Shari wanikingia, vitani wanitosha.

3

Nakutaka Mpaji, vyote napata kwako, Niwapo mhitaji, utanijazi vyako, Nao waangukao, wanyonge wape nguvu, Poza wauguao, uongoze vipofu.

4

Bwana umeniosha, moyo kwa damu yako, Neema ya kutosha, yapatikana kwako, Kwako Bwana naona, kisima cha uzima, Mwangu moyoni Bwana, bubujika daima.