4

Jina la Yesu, Salamu

1

Jina la Yesu, salamu! lisujudieni, Ninyi mbinguni, hukumu na enzi mpeni. Ninyi mbinguni, hukumu na enzi mpeni.

2

Enzi na apewe kwenu, watetea dini; Mkuzeni Bwana wenu, na enzi mpeni. Mkuzeni Bwana wenu, na enzi mpeni.

3

Enyi mbegu ya rehema, nanyi msifuni Mmeponywa kwa neema, na enzi mpeni. Mmeponywa kwa neema, na enzi mpeni.

4

Wenye dhambi kumbukeni, ya msalabani. Kwa furaha msifuni, na enzi mpeni. Kwa furaha msifuni, na enzi mpeni.

5

Kila mtu duniani msujudieni, Kote-kote msifuni, na enzi mpeni. Kote-kote msifuni, na enzi mpeni.

6

Sisi na wao pamoja tu mumo sifani. Milele sifa ni moja, ni enzi mpeni. Milele sifa ni moja, ni enzi mpeni.