1
Niimbe (niimbe) pendo lake, pendo la (pendo la) Yesu Bwana, Sababu (Sababu) alitoka, kwa Baba akafa.
Kiitikio
Niimbe (niimbe) pendo lake, sifa kuu (sifa kuu) nitatoa, Akafa (akafa) niwe hai, niimbe pendo lake.
2
Machozi (machozi) alitoa, ijapo (ijapo) sijalia, Maombi (maombi) yangu bado, aniombeapo.
3
Upendo (upendo) mkubwa huo! Dunia (dunia) haijui, Msamaha (samaha) kwa kosa, kubwa kama langu.
4
Hapana (hapana) tendo jema, ambalo (ambalo) nilitenda, nataka (nataka) toka leo, nimwonyeshe pendo.