32

Ninao Wimbo Mzuri

1

Ninao wimbo mzuri, tangu kuamini, Wa Mkombozi mfalme, tangu kuamini.

Kiitikio

Tangu kuamini, jina lake ‘tasifu, Tangu kuamini, nitalisifu jina lake.

2

Kristo anitosha kweli, tangu kuamini, Mapenzi yake napenda, tangu kuamini.

3

Nina ushuhuda sawa, tangu kuamini, Unalofukuza shaka, tangu kuamini.

4

Ninalo kao tayari, tangu kuamini; Nililorithi kwa Yesu, tangu kuamini.