1
Nipe habari za Yesu, kwangu ni tamu sana, Kisa chake cha thamani, hunipendeza sana, Jinsi malaika wengi, walivyoimba sifa, Alipoleta amani, kwa watu wa dunia.
Kiitikio
Nipe habari za Yesu, kaza moyoni mwangu, Kisa chake cha thamani, hunipendeza sana.
2
Kisa cha alivyofunga, peke yake jangwani, Jinsi alivyolishinda, jaribu la Shetani, Kazi aliyoifanya, na siku za huzuni, Jinsi walivyomtesa; yote ni ya ajabu.
3
Habari za Msalaba, aliposulubishwa, Jinsi walivyomzika akashinda kaburi, Kisa chake cha rehema, upendo wake kwangu, Aliyetoa maisha, nipokee wokovu.