35

Nimekombolewa na Yesu

1

Nimekombolewa na Yesu, na sasa nimefurahi, Kwa bei ya mauti yake, mimi ni mtoto wake.

Kiitikio

Kombolewa! Nakombolewa na damu, Kombolewa! mimi mwana wake kweli.

2

Kukombolewa nafurahi, kupita lugha kutamka, Kulionyesha pendo lake, mimi ni mtoto wake.

3

Nitamwona Mfalme wangu, katika uzuri wake, Ambaye najifurahisha, katika torati yake.

4

Najua taji imewekwa, mbinguni tayari kwangu, Muda kitambo atakuja, ili alipo niwepo.