1
Ni siku kuu, siku ile, ya kumkiri Mwokozi, Moyo umejaa tele, kunyamaza hauwezi.
Kiitikio
Siku kuu! Siku kuu! ya kuoshwa dhambi zangu kuu, Hukesha na kuomba tu, ananiongoza miguu, Siku kuu! siku kuu! ya kuoshwa dhambi zangu kuu.
2
Tumekwisha kupatana, mimi wake, yeye wangu, Na sasa nitamwandama, nikiri neno la Mungu.
3
Moyo tulia kwa Bwana, kiini cha raha yako, Huna njia mbili tena, uwe naye uendako.