5

Na Tumwabudu Huyo Mfalme

1

Na tumwabudu huyo Mfalme, Sifa za nguvu zake zivume; Ni ngao, ni ngome, Yeye milele, Ndizo sifa zake kale na kale.

2

Tazameni ulimwengu huu, Ulivyoumbwa, ajabu kuu; Sasa umewekwa pahali pake, Hata utimize majira yake.

3

Kwa ulinzi wako, kwetu Bwana, Twakushukuru, U mwema sana; Hupewa chakula kila kiumbe, Kila kitu kina mahali pake.

4

Wanadamu tu wanyonge sana, Twakutumaini Wewe, Bwana; Kamwe haupungui wako wema, Mkombozi wetu, Rafiki mwema.