1
Miguuni pake Yesu, maneno yake tamu, Pahali palipo heri, niwepo kila siku. Miguuni pake Yesu nakumbuka upendo Na hisani yake kwangu, vimenivuta moyo.
2
Miguuni pake Yesu, hapa mahali bora, Pa kuweka dhambi zangu, mahali pa pumziko. Miguuni pake Yesu, hapa nafanya sala, Kwake napewa uwezo, faraja na neema.
3
Unibariki Mwokozi, ni miguuni pako, Unitazame kwa upendo, nione uso wako. Nipe Bwana nia yake, ili ionekane, Nimekaa na Mwokozi, aliye haki yangu.