58

Leo Ninafikiria

1

Leo ninafikiria nchi nzuri, ninayotaka kuiona, Nisimamapo karibu na Mwokozi, tajini zitakuwa nyota?

Kiitikio

Sijui tajini mwangu kama nyota, zitang’aa kila wakati. Nitakapoamka katika majumba, zitakuwa nyota tajini?

2

Kwa nguvu za Bwana nitafanya kazi, nitavuta roho za watu, Ili niwe na nyota katika taji, Bwana anapotupa tunu.

3

Nitakuwa na furaha nikimwona, kuweka miguuni pake, Watu waliovutwa kwa ajili ya kazi yangu na roho yake.