1
Fanyeni kazi zenu, usiku si mbali, Kesheni saa zenu, vumilieni, Kwa Yesu tumikeni, na hiyo Injili, Sana wahubirini, watu wa mbali.
2
Fanyeni kazi zenu, giza lasogea, Na wengi wenzi wenu, wamo gizani, Msipoteze moja, dakika ni hizi, Bwana atarejea, mwisho wa kazi.
3
Fanyeni kazi zenu, hivi jua lachwa: Wote walio kwenu apenda Mungu Na sisi tumjuaye na tuwafundishe Ili Yesu ajaye tumfurahishe.