1
Pengine siyo mlimani, utakaponiita, Pengine siyo baharini, wala palipo vita, Lakini unaponiita, na njia siijui, Bwana nitajibu ni tayari, kwenda uniagizapo.
Kiitikio
Ukiwa pamoja nami Bwana, mlimani baharini, Niende utakaponiita; na fuata uendako.
2
Pengine leo kuna neno, neno tamu la pendo, Ambalo Yesu anataka, ninene kwa upole, Ukiwa pamoja nami Bwana, nitamtafuta leo, Yule aliyepotea mbali, nitasema upendavyo.
3
Pahali pako bila shaka, pa kuvuna shambani, Kazi niwezayo kufanya, kwa Yesu Mkombozi, Hivi nikikutegemea, kwa kuwa wanipenda, Mapenzi yako nitayafanya, na niwe upendavyo.