1
Nimemwona rafiki, wa thamani kubwa, Ananipenda kwa ‘pole, kwa pendo amini, Kuishi kutengwa naye, la, huku siwezi, Tunakaa pamoja, Bwana nami.
2
Pengine ninachoka, mimi mdhaifu, Ndipo ninamtegemea, alivyoalika, Huniongoza njiani, pahali pa nuru, Twatembea pamoja Bwana nami.
3
Namweleza huzuni, mimi mdhaifu, Vile vinavyosumbua, vinavyopendeza, Huniagiza kutenda, yanayonipasa, Twatembea pamoja, Bwana nami.
4
Ajua natamani, kuwavuta watu, Hivyo ananipeleka, kutangaza Neno, Nitangaze pendo lake, kwa nini akafa, Twahubiri pamoja, Bwana nami.