62

Napenda Kitabu Chake

1

Napenda kitabu chake, kilichotoka mbinguni, Barua kwangu ya Bwana, ujumbe wake wa pendo.

2

Humo ndani ya kitabu, sura ya Yesu naona, Karatasi zimekuwa, nyayo zake za kiongozi.

3

Neno lake tamu sana, kama asali naona, Natamani kulionja, ni mkate wa uzima.

4

Mapenzi yake mwumbaji, yanafunuliwa humo, Hazina kuu ya hekima, utajiri wa ajabu.

5

Mwangaza wa ulimwengu, angaza humo moyoni, Uwe mwandamizi pote, taa ya hatua zangu.