1
Niuonapo Msalaba, Kristo aliponifia, Kwangu pato ni hasara, kiburi nakichukia.
2
Na nisijivune Bwana, ila kwa sadaka yako, Upuzi sitaki tena, zi chini ya damu yako.
3
Tazama kichwani kwake, mikononi na miguu, Huzuni pendo twaona, vyabubujika daima.
4
Vitu vyote vya dunia, si sadaka ya kutosha, Pendo zako zaniwia, nafsi mali na maisha.