64

Piga Panda ya Injili

1

Piga panda ya injili, onyesha watu wote, Ili anayesikia, atubu aokoke.

Kiitikio

Piga panda ya injili, uipige kwa nguvu, Mungu amekuagiza, mateka wawe huru.

2

Uipige vilimani, kwa kila tambarare, Pande zote miji yote, isikie injili.

3

Uipige mipakani, barabarani pia, Iwatangazie wote, wanaitwa na Baba.

4

Uipige watu wengi, wataka wawe huru, Waambie kwamba Yesu, asema “Njoni kwangu.”