1
Twendeni askari watu wa Mungu, Yesu yuko mbele, tumwandame juu, Ametangulia Bwana vitani, twende mbele kwani ndiye amini.
Kiitikio
Twendeni askari, watu wa Mungu, Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
2
Jeshi la Shetani likisikia, jina la Mwokozi litakimbia, Kelele za shangwe zivume pote, ndugu inueni zenu sauti.
3
Kweli kundi dogo watu wa Mungu, la watakatifu ni letu fungu, Hatutengwi nao moja imani, tumaini moja na moja dini.
4
Haya mbele watu nasi njiani, inueni mioyo nanyi sifuni, Heshima na sifa yake Mfalme. juu hata chini sana zivume.