66

Roho Yangu Amka Sasa

1

Roho yangu amka sasa, mara jitahidi, Shindano ni lake Bwana, zawadi ni taji.

2

Sauti ni yake Mungu inayokuita, Ndiyo aliyekirimu, taji ya uzima.

3

Mashahidi ndio wengi, wanaokuona, Ya nyuma usifikiri, bali mwendo kaza.

4

Bwana umetuanzisha, katika shindano, Kwa vile tunaposhinda, ushindi ni wako.