1
Umtetee Mungu duniani, ijapo pepo kali zavuma, Mwambani pekee pana nguvu, dhambi ikilemea.
Kiitikio
Tusimame imara katika mwamba, Mwamba wa Kristo pekee, Ndipo salamani tutasimama, Kule kitini pa enzi.
2
Itetee haki kwa bidii, kwa moyo mnyofu wa imani, Mwambani pekee utashinda, wingi wa upotovu.
3
Itetee kweli itadumu, ijapokawia itashinda, Mwambani pekee pana raha, yaishapo tufani.