1
Cha kutumaini sina, ila damu yake Bwana, Sina wema wa kutosha, dhambi zangu kuziosha.
Kiitikio
Kwake Yesu, nasimama, Ndiye mwamba, ni salama, Ndiye mwamba, ni salama.
2
Njia yangu iwe ndefu, yeye hunipa wokovu, Mawimbi yakinipiga, nguvu zake ndiyo nanga.
3
Damu yake na sadaka, nategemea daima, Yote chini yakiisha, Mwokozi atanitosha.
4
Nikiitwa hukumuni, rohoni nina amani, Nikivikwa haki yake, sina hofu mbele zake.