70

Wapenzi wa Bwana

1

Wapenzi wa Bwana, ije raha yenu, Imbeni nyimbo za raha, imbeni nyimbo za raha, Za ibada yenu, za ibada yenu.

Kiitikio

Twenenda Zayuni, mji mzuri Zayuni, Twenenda juu Zayuni, Ni maskani ya Mungu.

2

Wasiimbe wao wasioamini, Watoto wa Mungu ndio, watoto wa Mungu ndio, Waimbao chini, waimbao chini.

3

Twaona rohoni, baraka za Mungu, Tusijafika mbinguni, tusijafika mbinguni, Kwenye utukufu, kwenye utukufu.

4

Tutakapomwona, masumbuko basi, Huwa maji ya uzima, huwa maji ya uzima. Furaha halisi, furaha halisi.