1
Mungu Msaada wetu, tangu miaka yote, Ndiwe tumaini letu, la zamani zote.
2
Kivuli cha kiti chako, ndiyo ngome yetu, Watosha mkono wako, ni ulinzi wetu.
3
Kwanza havijakuwako, nchi na milima, Ndiwe Mungu, chini yako twakaa salama.
4
Na miaka elfu ni kama, siku moja kwako; Utatulinda daima, tu raia wako.
5
Bwana Msaada wetu tangu miaka yote, Mlinzi wetu na ngome, daima, milele.