8

Unisikie Ninapolia

1

Unisikie ninapolia, uje Mkombozi, Moyo wangu hukutazamia, uje Mkombozi.

Kiitikio

Nimepotea mbali na kwangu, nimetanga peke yangu, Unichukulie sasa kwako, uje Mkombozi.

2

Sina pahali pa kupumzika, uje Mkombozi, Unipe raha, nuru, uzima, uje Mkombozi.

3

Nimechoka, Njia ni ndefu uje Mkombozi, Macho yako kuona nataka, uje Mkombozi.

4

Bwana, daima hutanidharau, uje Mkombozi, Kilio changu utanijibu, uje Mkombozi.