1
Kesha ukaombe, panapo nafasi, Wakati si mwingi, kwa hiyo ukeshe, Mwili ni dhaifu, adui hodari, Karibu atakuja, Bwana wa arusi.
Kiitikio
Kesha, Omba, Kesha, Omba, Kesha kaombe gizani, mchana daima kesha.
2
Fukuza usingizi, fukuza mashaka, Ahadi ni yako, raha ya milele, Bwana alikesha, kwa ajili yako, Jasho lake likawa, matone ya damu.
3
Yesu umkubali, awe nguvu zako, Silaha uzivae, adui karibu, Sasa nafasi iko, isipite bure, Bila kukawia, Masihi yuaja.