72

Jenga Juu ya Mwamba

1

Tutajenga juu ya mwamba, wa Yesu mwamba wa kale, Tutavumilia kishindo, tufani ivumapo.

Kiitikio

Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu) Tutajenga juu, (Tutajenga juu ya mwamba mkuu) Tutajenga juu ya mwamba mkuu, juu yake Yesu.

2

Wengine hujenga katika, mchanga wa ulimwengu, Wengine katika mawimbi, ya anasa za dhambi.

3

Jenga nawe juu ya mwamba, msingi pekee wa kweli, Tumai lake litadumu, tumai la wokovu.