1
Nakaza mwendo mbinguni, kila siku napanda juu, Naomba nikisafiri, Bwana uniongoze juu.
Kiitikio
Bwana uniinue juu, kwa imani hata mbingu, Juu kuliko dunia, Bwana uniongoze juu.
2
Moyo wangu hautaki, kukaa palipo shaka, Wengine wapenda chini, nia yangu ni kupanda.
3
Nataka kupanda juu, nisishindwe na adui, Kwa imani nasikia, sauti ya washindaji.
4
Kupanda juu nataka, niuone utukufu, Hata mwisho nitaomba, Bwana uniongoze juu.