Niambie Ee mlinzi, je, kumepambazuka , Utukufu wa Zayuni, pana dalili zake? Msafiri uondoke, utazame mbinguni, Kiunoni ujifunge, ni kucha alfajiri.
Mlinzi, inamulika, nuru njiani mwako, Dalili za kuja kwake, kwamba siku karibu, Panda itakapolia, itawaamsha wafu, Watakatifu wa Mungu, kuwapa kutokufa.
Mlinzi ione nuru, ya mwaka wa Sabato, Sauti zinatangaza, ufalme ni karibu, Msafiri ninaona, mlima wa zayuni, Mji wa Yerusalemi, nayo fahari yake.
Kwenye mji wa dhahabu, anaketi Mfalme, Katika kiti kizuri, huku anatawala, Pana amani po pote, mashamba husitawi, Na ardhi ina rutuba; mito ni mitulivu.
Mlinzi twakaribia, nchi iliyo nzuri, Twende mbele tufurahi, nchi inachangamka, Sikieni kuna wimbo, wa waliookoka, Kaza mwendo ujiunge, na kundi kubwa hili.