1
Msingi imara ninyi wa Bwana, Umewekwa kwenu kwa neno lake, Nini zaidi atasema Bwana, Imani yenu ipate kuzidi?
2
Wambiwapo vuka maji ya giza, Mito ya mashaka haitazidi, Takuwapo nawe nikuwezeshe, Shida upatazo zisikutishe,
3
Utakapopishwa ndani ya moto, Nguvu nitakupa, upate pato, Huteketezwi ila taka zako, Na zitasalia dhahabu zako.
4
Na mtu aliyenitegemea, Nguvu za Jehanamu zijapotisha, Kamwe kwa adui sitamtia, Mtu wangu kamwe sitamuacha.