76

Mrithi Ufalme

1

Mrithi ufalme kwani walala? Karibu wokovu wasinzia? Amka simama uvae silaha, Haraka sana saa zapita.

2

Mrithi ufalme mbona ‘kawia? Mbona hupokei zawadi? Haya uvae Mwokozi yuaja, Haraka umlaki afikapo.

3

Mataifa makuu ya dunia, Yapigana na kujiangusha, Usizihofu dalili, mrithi, Ishara zote hazikawii.

4

Sitazame anasa za dunia, Kwani hayo yapita upesi, Zivunje kamba zinazokufunga, Mrithi ufalme njoo karudi.

5

Inua kichwa tazama mbele tu, Mfalme aja na utukufu, Jua laonekana milimani, Warithi ufalme furahini.