77

Je! Mlinzi Ukutani

1

Je mlinzi ukutani, wa mji wa Zayuni, Habari zake usiku, asubuhi karibu? Kuna dalili za kupambazuka? Kuna dalili za kupambazuka?

2

Katika safari yetu, twaona nchi kavu? Tutalala baharini, bandari bado mbali? Kweli kweli, tutaona ufalme? Kweli kweli, tutaona ufalme?

3

Tunaona nuru yake, nyota ya asubuhi, Nyota tukufu na safi, inang’aa mbinguni, Furahini, wokovu u karibu, Furahini, wokovu u karibu.

4

Tumetazama ramani, kweli pwani si mbali, Twende mbele, kwa upesi tutaona bandari, Furahani, imbeni nyimbo zenu, Furahani, imbeni nyimbo zenu.