79

Nataka Imani Hii

1

Nataka imani hii, imani imara, Ambayo haitetemi kitu chote wakati wa shida, Wakati wa shida.

2

Isiyonung’unikia, huzuni taabu; Lakini katika saa ya matata humwamini Mungu, Humwamini Mungu.

3

Imani inayong’aa, katika tufani, Isiyoogopa giza wala shida njaa na hatari, Njaa na hatari.

4

Haiogopi dunia, kudharau kwake, Haiangushwi na hila, nayo dhambi na udanganyifu, Na udanganyifu.

5

Bwana nipe imani hii, hivi nitaweza Kuonja hapa chini ulimwenguni kurithi furaha, Kurithi furaha.