1
Tupe moto wa uhai, uliowaka zamani, Uliowaongoza juu, wazee watakatifu.
2
Wapi roho iliyokaa, moyoni mwa Ibrahimu? Kadhalika ndugu Paulo, aliwezeshwa na moto.
3
Kwani neema haina, nguvu siku hizi sawa, Kama wakati wa Musa, Ayubu na wa Eliya?
4
Zamani za kale Bwana, kumbuka na kwa rehema, Zihuishe roho zetu, kwa Roho Mtakatifu.