81

Siku Sita Zimepita

1

Siku sita zimepita, Sabato tena karudi, Shangilie roho yangu, itukuze kwa busara.

2

Msifuni awapaye, pumziko tamu wachovu, Kwake roho yatulizwa, kupita siku nyingine.

3

Moyo wetu ufurahi, na kutoa shukurani, Ujalizwe raha ile, yasiyopitika kamwe.

4

Raha hiyo ya rohoni, ni amana ya pumziko, Ambalo limewekwa juu, kikomo cha masumbuko.