82

Ni Siku ya Furaha

1

Ni siku ya furaha, ni siku ya nuru, Nasi twaona raha, kuja kushukuru, Leo watu wa Mungu, wadogo wakubwa, Hukaribia mbingu, ilipo baraka.

2

Leo ndiyo bandari, nasi twawasili, Hiyo bustani nzuri, ya nyingi fadhili, Kijito cha baridi, kimefanya ziwa, Na kiu ikizidi, twanywa maridhawa.

3

Leo ngazi na iwe, ifikayo juu, Mawazo na yasiwe, ya duniani tu, Leo ni kujilisha, chakula cha mbingu, Na kujifurahisha, kwa mambo ya Mungu.