1
Kaa nami, ni usiku tena, usiniache gizani, Bwana, Msaada wako haukomi, nili peke yangu, kaa nami.
2
Siku zetu hazikawi kwisha, sioni la kunifurahisha, Hakuna ambacho hakikomi, usiye na mwisho kaa nami.
3
Nina haja nawe kila saa, sina mwingine wa kunifaa, Mimi nitaongozwa na nani, ila wewe Bwana kaa nami.
4
Sichi neno uwapo karibu, nipata lo lote si taabu, Kifo na kaburi haviumi, nitashinda kwako kaa nami.
5
Nilalapo nikuone wewe, gizani mote nimulikiwe, Nuru za mbinguni hazikomi, siku zangu zote, kaa nami.