1
Magharibini jua, limekwisha kushuka, Mwezi na nyota sasa, vinamsifu muumba wa usiku .
Kiitikio
Mungu Mtukufu, Mungu mkuu, Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu.
2
Mpaji wa uhai, ukaaye mbinguni, Utuhifadhi sisi, tufahamu gizani u karibu.
3
Mapenzi yako makuu, yawe nasi usiku, Tuli usingizini, kucha vivyo rohoni tushukuru.
4
Na utakapokuja, na nguvu kutawala, Mungu wangu kubali, kunipeleka mimi uliko juu.
5
Baba Mwana Roho, Mungu wetu, Wote juu mbinguni, na wanadamu chini twakusifu.