93

Jua la Rohoni Mwangu

1

Jua la rohoni mwangu, mpendwa Mwokozi wangu, Usiku giza hapana, ukiwa karibu Bwana.

2

Nikipata usingizi, nijaze fikara hizi, Ni tamu sana, nilale pendoni mwako milele.

3

Kaa nami ewe Bwana, usiku kama mchana, Nisiishi mbali nawe, ni uhai kuwa nawe.

4

Kama mtoto mnyonge, ameshawishwa atange, Mtafute ewe Bwana, ujirudishie tena.

5

Wagonjwa wape amani, waneemeshe maskini, Waliao, Mtulizi, wape wote usingizi.

6

Asubuhi tutokapo, tukaribie tulipo, Twingiapo duniani, tuwe mwako mkononi.