94

Po pote Mashamba Yajaa

1

Po pote mashamba yajaa, tele nafaka pevu, Po pote yang’aa meupe, bondeni na nyandani.

Kiitikio

Mwenye mavuno twasihi, upeleke wavuni, Wayakusanye mazao, hata kazi yaishe.

2

Wapeleke uchaoni, waende na jotoni, Hata jua lishukapo, wakusanye ko kote.

3

Enyi wakazi wa bwana, yaleteni mazao, Na jioni ingieni, kwake na furaha kuu.