95

Sikieni Neno

1

Sikieni neno la Mungu wetu, zileteni zaka kwa hazina Leteni na mioyo yenu yote, mibaraka itakuja.

Kiitikio

Zileteni zaka kwa hazina, kanijaribu sasa nazo, Nitakupeni mibaraka, zaidi ya nafasi ya kupewa.

2

Wataka Roho Mtakatifu kwako? Uzilete zaka kwa hazina Ukae karibu na Bwana wako, ndipo utabarikiwa.

3

Je, una kasoro na Bwana wako? Uzilete zaka kwa hazina, Uzilete kama alivyosema, ndipo utabarikiwa.

4

Ushukuru Bwana na moyo wote, unapoleta zaka ghalani, Usadiki ahadi zake zote, ndipo utabarikiwa.

5

Tuimbe sote nyimbo za furaha, tunapoleta zaka ghalani, Tuimbe kabisa na furaha kubwa, kwani tutabarikiwa.